Awamu ya tano ya kufukuliwa miili katika msitu wa Shakahola
4 Juni 2024Awamu hiyo ya tano ilianza tena mapema wiki hii na waziri wa usalama nchini Kenya Kithure Kindiki. Kufikia sasa idadi ya miili iliyofukuliwa kwa jumla imefikia 436.
Makaburi mengine 50 yamepatikana na shughuli ya kufukuwa inaendelea. Daktari Mkuu wa Serikali, Johansen Oduor, ameeleza kuwa miili hiyo saba imepatikana kwenye makaburi manne, huku miili minne ikipatikana imezikwa kwenye kaburi moja.
Soma pia:Miili ya wahanga wa Shakahola yatolewa kwa familia Kenya
Daktari Oduor ameeleza pia kuwa makaburi hayo yametambuliwa kwa urahisi kutokana na udongo kuwa mwepesi.
Paul Mackenzie, mhubiri aliyekamatwa kwa madai ya kuwalazimisha wafuasi wake kujizuia kula na kunywa hadi kufa pamoja na washukiwa wengine 94 ambao bado wanazuiliwa katika gereza la shimo la tewa mjini Mombasa.