1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Ayatollah aionya Marekani dhidi ya kuishambulia Iran

17 Februari 2026

Kiongozi wa juu zaidi wa Iran Khamenei ameionya Marekani wakazi duru ya pili ya mazungumzo kuhusu Nyuklia ikifanyika Geneva

Kiongozi wa juu zaidi nchini Iran Ayatollah Ali Khamenei akihutubia mjini Tehran
Kiongozi wa juu zaidi nchini Iran Ayatollah Ali KhameneiPicha: Office of the Iranian Supreme Leader/WANA/REUTERS

Duru ya pili ya mazungumzo yasiyo ya moja kwa moja kati ya Iran na Marekani imemalizika mjini Geneva chini ya usimamizi wa Oman, kwa mujibu wa vyombo vya habari vya Iran.

Waziri wa mambo ya nje wa Iran Abbas Aragchi amesema mazungumzo hayo yametowa fursa ya mataifa hayo mawili kukubaliana juu ya taratibu za muongozo utakaofungua njia ya kupatikana makubaliano.

Muda mfupi kabla ya kuanza mazungumzo hayo, kiongozi wa juu zaidi wa Iran Ayatollah Ali Khamenei alimuonya rais Donald Trump akimwambia hawezi kuiangusha Jamhuri hiyo ya kiislamu.

"Tunawasikia kila mara wakisema kwamba wao (Marekani) wamepeleka manuari za kivita kuelekea Iran. Manuari ya kivita bila shaka ni silaha hatari lakini kilichokuwa hatari zaidi ni ile silaha yenye uwezo wa kuizamisha mpaka chini ya bahari hiyo manuari ya kivita''

Kauli hiyo ya Khamenei ameitowa kwenye hotuba yake  hivi leo siku chache baada ya rais wa Marekani Donald Trump kusema mabadiliko ya kiutawala ni kitu muhimu kinachopaswa kufanyika Iran. Iran na Marekani kuendeleza mazungumzo Uswisi Jana Jumatatu  Tehran ilianzisha luteka ya kijeshi katika mlango bahari wa Hormuz, ambayo ni njia muhimu ya safari za meli za Mafuta.

 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW