1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Ayatollah Ali Khamenei awaongoza Wairan kumuaga Raisi

22 Mei 2024

Kiongozi wa Juu wa Iran Ayatollah Ali Khamenei, ameongoza mjini Tehran, ibada ya kumswalia na kutowa heshima za mwisho kwa rais Ebrahim Raisi,

Siasa za Iran Ali Khemenei na Ebrahim Raisi
Kiongozi wa kidini wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran, Ali Khamenei (kushoto) akizungumza na aliyekuwa rais wa taifa hilo marehemu Ebrahim Rais.Picha: leader.ir

Ibada hiyo pia imewahusisha waziri wake wa mambo ya nje Hossein Amir-Abdollahian na maafisa wengine wa serikali waliofariki dunia kufuatia ajali ya helikopta Magharibi mwa Iran. 

Ibada hiyo imefanyika katika chuo kikuu cha Tehran ambako majeneza ya viongozi hao yalifunikwa kwa bendera ya Taifa na picha zao kuwekwa juu yake. Kaimu rais wa Iran Mohammad Mokhber aliyesimama muda wote kando na Khamenei alibubujikwa machozi wakati ibada hiyo ikiendelea.

Kiongozi wa Hamas Ismail Haniyeh alishiriki kwenye ibada hiyo. Haniyehamesema amefika katika ibada hiyo kutoa risala zake za rambi rambi pamoja na watu Palestina kwa Iran kwa kuwapoteza viongozi wao muhimu. Iran imekuwa ikiiunga mkono Hamas katika vita vyake na Israel katika Ukanda wa Gaza.