1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaAzerbaijan

Azerbaijan, Armenia mbioni kufikia makubaliano ya amani

Sylvia Mwehozi
23 Aprili 2024

Rais wa Azerbaijan Ilham Aliyev ameelezea matumaini makubwa ya kufikiwa makubaliano ya amani na Armenia kuliko ilivyokuwa hapo awali.

Rais wa Azerbaijan Ilham Aliyev na Waziri Mkuu wa Armenia Nikol pashinyan
Rais wa Azerbaijan Ilham Aliyev na Waziri Mkuu wa Armenia Nikol pashinyanPicha: Vladimir Smirnov/Sputnik/AP/picture alliance

Timu kutoka nchi hizo mbili zitaweka alama kwenye mpaka kulingana na ramani za enzi ya Kisovieti. Rais Aliyev ameongeza kuwa.

"Hatukuwa na rasimu ya makubaliano ya amani wakati huo, lakini sasa tunayo. Sasa tuna uelewa wa pamoja wa jinsi makubaliano ya amani yanapaswa kuwa. Tunahitaji tu kushughulikia maelezo".

Waziri Mkuu wa Armenia Nikol Pashinyan mwezi uliopita alikubali ombi la Azerbaijan la kurudisha vijiji vinne vya mpaka ambavyo vilikuwa sehemu ya Azerbaijan wakati nchi hizo mbili zilipokuwa Jamhuri za Muungano wa Kisovieti.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW