1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Azerbaijan inafanya uchaguzi wa bunge

1 Septemba 2024

Azerbaijan nafanya uchaguzi ulioharakishwa wa bunge, ukiwa ni wa mwanzo tangu taifa hilo la lililokuwemo katika uliokuwa umoja wa kisoviet lipate udhibiti wa mtengamano baada ya mashambulizi makali ya mwaka uliopita.

Aserbaidschan | Putins Besuch
Rais wa Azerbaijan Ilham Aliyev, kulia, akisalimiana na Rais wa Urusi Vladimir Putin, kushoto, kwenye makazi ya jimbo la Zagulba huko Baku, Azerbaijan, Agosti 19, 2024. Picha: Grigory Sysoyev/Sputnik/Kremlin/AP Photo/picture alliance

Chaguzi zilizopita tangu liwe huru kutoka kwa umoja huo hazikuwa zikitazamwa kama huru au za haki, na matokeo yake kwa Milli Mejlis bunge la taifa hilo  hayatarajiwi kuleta mabadiliko muhimu kwa chombo hicho ambacho ambacho kinadhibitiwa na chama cha Rais Ilham Aliyev cha New Azerbaijan.

Chama hicho tawala kinashikilia viti 69 kati ya 125bungeni, na wengi waliosalia ni wa vyama vidogo vinavyounga mkono serikali au kujitegemea.Chama cha Musavat, chama kikuu cha upinzani, kilitoa wagombea 34 wa uchaguzi wa huu lakini  kati ya hao 25 tu waliruhusiwa kushiriki.

Baba ya Rais Aliyev alitawala Azabajan kuanzia 1993 hadi alipofariki mwaka 2003, ambapo Ilham akachukua nafasi. Wote wawili wanatazamwa kuongoza taifa hilo lenye jumla ya watu milioni 10 kimabavu.

 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW