1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Azerbaijan na Armenia kuzungumza kuhusu Nagorno Karabakh

26 Septemba 2023

Wajumbe kutoka Arzebaijan na Armenia watakutana leo mjini Brussels, Ubelgiji, kwa majadiliano kuhusu mgogoro wa jimbo la Nagorno Karabakh, wakati jumla ya wakimbizi 13,350 wakiwa wamewasili Armenia.

Polisi wa Armenia wakiwapokea na kuwaratibu wakimbizi kutoka Nagorno Karabakh
Polisi wa Armenia wakiwapokea na kuwaratibu wakimbizi kutoka Nagorno KarabakhPicha: Irakli Gedenidze/REUTERS

Maafisa wa Nagorno Karabakh pia wamearifu kwamba watu wasiopungua 20 wameuwawa na wengine takriban 300 wamejeruhiwa kufuatia mripuko uliotokea katika kituo cha kujaza gesi wakati watu wakihangaika kukimbilia Armenia.

Soma pia:Maelfu wahama Nagorno-Karabakh kukimbilia Armenia

Mkutano huo utakuwa wa kwanza unaozikutanisha pande zote mbili tangu ilipoanza operesheni ya kijeshi ya Azerbaijan, ingawa viongozi wa juu wa nchi hizo mbili wamepangiwa kukutana mwezi ujao.

Mkutano wa Brussels utaongozwa na  Simon Mordue, ambaye ni mshauri mkuu wa masuala ya kidiplomasia wa rais wa baraza la Umoja wa Ulaya, Charles Michel. Ujerumani na Ufaransa pia zitawakilishwa kwenye mkutano huo.

 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW