1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaAsia

Azerbaijan na Armenia kusitisha mapigano ya Nagorno-Karabakh

20 Septemba 2023

Ripoti zimesema makubaliano hayo yametangazwa na mamlaka za jimbo hilo nchini Arzebaijan.

Makubaliano hayo yalifikiwa kupitia usimamizi wa walinda amani wa Urusi kwenye jimbo hilo.
Makubaliano hayo yalifikiwa kupitia usimamizi wa walinda amani wa Urusi kwenye jimbo hilo. Picha: Karen Minasyan/AFP/Getty Images

Vyombo vya habari vya Armenia vimeripoti hii leo juu ya kufikia makubaliano ya kusitisha mapigano na Arzebaijan, yaliyodumu kwa siku mbili baada ya Arzebaijan kuanzisha operesheni ya kijeshi dhidi vikosi vya jimbo lililojitenga la Nagorno-Karabakh.

Ripoti hizo zimesema makubaliano hayo yametangazwa na mamlaka za jimbo hilo nchini Arzebaijan na yataanza kutekelezwa majira ya saa saba mchana ya eneo hilo hii leo. 

Chini ya mkataba huo, vikosi vya Armenia vimetakiwa kuondoka Nagorno-Karabakh pamoja kuvipokonya silaha vikosi vya ulinzi kwenye eneo hilo. 

Kulingana na Armenia mapema leo, karibu watu 32 wameuawa na wengine wengi wamejeruhiwa licha ya miito ya Urusi na Marekani ya kusitisha mapigano. 

Soma pia:

Armenia imeishutumu Azerbaijan kwa 'uchokozi wa kijeshi'

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW