Azerbaijan na Armenia zatuhumiana kushambuliana mpakani
13 Februari 2024Matangazo
Wizara ya Ulinzi ya Armenia imesema askari wa Azerbaijan walifyetua risasi kuvilenga vituo vya wanajeshi wake kwenye kijiji cha Nerkin Hand na kusababisha vifo hivyo vya wanajeshi na kujeruhiwi wengine.
Hata hivyo walinzi wa mipaka wa Azerbaijan wamesema mashambulizi yao yalikuwa yakijibu uchokozi wa wanajeshi wa Armenia ambao wanasema walimjeruhi askari mmoja wa nchi hiyo. Hayo ni makabiliano ya hivi karibuni kabisa baina ya wanajeshi wa pande hizo mbili ambao wako kwenye hali ya tahadhari wakati wote.
Nchi hizo mbili zilizokuwa sehemu ya Dola ya Kisovieti zimepiga vita mbili mnamo miaka 1990 na mwaka 2020 kuwania jimbo la Nagorno Karabakh ambalo Azerbaijan ililidhibiti kikamilifu mwaka uliopita.