1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaAzerbaijan

Azerbaijan yafanya uchaguzi wa rais

7 Februari 2024

Raia wa Azerbaijan wanapiga kura siku ya Jumatano kumchagua rais atakayeliongoza taifa hilo.

Picha ya Kampeni ya Rais wa Azerbaijan Ilham Aliyev
Mtu akipita karibu na Picha ya Kampeni ya Rais wa Azerbaijan Ilham Aliyev mjini Baku:07.02.2024Picha: Sergei Grits/AP/picture alliance/dpa

Rais wa sasa na mwenye ushawishi mkubwa Ilham Aliyev anatazamiwa kwa kiasi kikubwa kujishindia muhula wa tano madarakani.

Ukandamizaji wa vyombo huru vya habari na kutokuwepo upinzani wowote wa kweli dhidi ya Aliyev, vinamuongezea uhakika wa kupata ushindi wa kishindo. Mwezi Septemba mwaka jana, Vikosi vya Baku vilichukua tena udhibiti wa eneo linalozozaniwa la Nagorno-Karabakh.

Vyama vikuu vya upinzani katika taifa hilo lenye utajiri mkubwa wa mafuta vimesusia uchaguzi huo. Kiongozi wa chama cha upinzani cha National Front, Ali Kerimli ameutaja uchaguzi huo kama "maigizo ya demokrasia" na kusisitiza kwamba hali ya sasa nchini Azerbaijan, hairuhusu kufanyika kwa uchaguzi huru na wa haki.