1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Azerbaijan yashtumu mataifa ya Magharibi kwa kuiharibia sifa

12 Novemba 2024

Rais wa Azerbaijan Ilham Aliyev, amevishtumu vyombo vya habari vya Magharibi akiviita ni vya kutoa taarifa za uongo pamoja na mashirika ya kimazingira kwa kampeni yao ya kuichafulia jina nchi yake.

Rais wa Azerbaijan, Ilham Aliyev akizungumza wakati wa kongamano la 74 la kimataifa kuhusu sayansi ya uundaji wa vyombo vya kusafiri angani mjini Baku mnamo Oktoba 2,2023
Rais wa Azerbaijan, Ilham AliyevPicha: Azerbaijani Presidency/AA/picture alliance

Akihutubia mkutano huo wa COP29 mjini Baku, Rais Aliyev, amesema wale wanaosema uchumi wa taifa lake unategemea zaidi uchimbaji na usafirishaji wa mafuta au gesi asilia, wanaonyesha ukosefu wa ufahamu.

Rais Aliyev ameongeza kuwa ilikuwa sawa kusema hivyo katika karne ya 19, wakati nchi hiyo ilichangia zaidi ya nusu ya uzalishaji wa mafuta duniani, lakini kusema hivyo sasa kunaonesha tu ukosefu wa utamaduni wa kisiasa na ufahamu.

Aliyev asema akiba ya mafuta na gesi ya Azerbaijan ni "zawadi ya Mungu"

Aliyev alirejelea mtazamo wake unaoibuwa utata kwamba akiba ya mafuta na gesi ya Azerbaijan ni "zawadi ya Mungu" na nchi hazipaswi kulaumiwa kwa kuzimiliki na pia hazipaswi kulaumiwa kwa kuleta rasilimali hizo sokoni kwa sababu soko linazihitaji, na wananchi wanazihitaji.

Mkutano wa kilele wa mazingira COP29 waanza Azerbaijan

Kwenye mkutano huo wa COP29 mjini Baku waziri mkuu wa Uingereza Keir Starmer nae ameahidi kuchukua hatua kubwa zaidi kufikia lengo la nchi yake la kupunguza gesi inayochafuwa mazingira akisema uzalishaji wa gesi chafuzi utapunguzwa kwa asilimia 81 ikilinganishwa na viwango vya 1990 ifikapo mwaka 2035 huku serikali yake ikiimarisha azma yake juu ya mabadiliko ya tabianchi.

Mahakama ya rufaa ya Uholanzi yabatilisha uamuzi dhidi ya kampuni ya mafuta ya Shell

Wakati wajumbe wakijadili kuhusu hatua za kuchukuliwa kuuokowa ulimwengu na mabadiliko ya tabia nchi mjini Baku, mahakama ya rufaa nchini Uholanzi leo imebatilisha uamuzi wa kihistoria ulioiamuru kampuni ya mafuta ya Shell kupunguza uzalishaji wake wa hewa chafu ya kaboni kwa asilimia 45 ifikapo mwaka 2030 ikilinganishwa na viwango vya mwaka 2019, huku ikisema kwamba ulinzi dhidi ya mabadiliko hatari ya tabianchi ni haki ya kibinadamu.

Kampuni ya mafuta ya ShellPicha: Robin Utrecht/picture alliance

Uamuzi huo ni pigo kwa tawi la Uholanzi la mtandao wa kimataifa wa mashirika ya mashinani ya harakati za kulinda kimazingira katika nchi 73 Friends of the Earth, pamoja na makundi mengine ya kimazingira ambayo yalisifu uamuzi wa awali wa mwaka 2021 walioutaja kuwa ushindi kwa mazingira.

Guterres: Athari za mabadiliko ya tabia nchi ni kubwa

Mkuu wa Friends of the Earth nchini Uholanzi Donald Pols, amesema uamzi huo unaumiza. Amesema kesi hiyo imeonesha kwamba makampuni wachafuzi wakubwa wa mazingira yanaweza pia kuchukuliwa hatua lakini pia kesi hiyo  imechochea zaidi mjadala kuhusu wajibu wao  katika kupambana na mabadiliko hatari ya tabianchi.

Guterres: Tuendelee kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi

Uamuzi huo pia uliashiria kushindwa pakubwa kwa wanaharakati wa kutetea mazingira  baada ya ushindi kadhaa  mahakamani. Mnamo mwaka 2015, mahakama ya The Hague iliiamuru serikali ya Uholanzi kupunguza uzalishaji wahewa chafuzi kwa angalau asilimia 25 ifikikapo mwishoni mwa mwaka 2020, kwa kuzingatia viwango vya 1990.

 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW