Azimio dhidi ya Syria
5 Oktoba 2011Matangazo
Azimio hilo lilipokea kura 9 za kuliunga mkono na wanachama wanne walikataa kupiga kura.
Urusi na China zilikuwa ni wanachama wa pekee waliopiga kura ya kupinga azimio hilo lililoandikwa na Ufaransa kwa ushirikiano na Uingereza, Ujerumani na Ureno.
Mataifa ya Ulaya yalipendekeza azimio ambalo litatishia kuchukuliwa hatua zilizolengwa iwapo rais Bashar al Assad hatositisha msako wake mkali katika muda wa siku 30.
Mwandishi Maryam Abdalla/dpa ap rtr afp