1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Azimio kuhusu vita vya Gaza kupigiwa kura

22 Desemba 2023

Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa linatarajiwa kulipigia kura leo azimio lililocheleweshwa kwa muda mrefu kuhusu vita vya Israel na Hamas.

USA, New York | Tagung des UN-Sicherheitsrats
Picha: Yuki Iwamura/AFP/Getty Images

Hii ni baada ya Marekani kuashiria kuliunga mkono kufuatia upinzani dhidi ya mapendekezo ya rasimu ya awali. Kura hiyo kwa mara nyingine iliahirishwa jana. Baada ya siku kadhaa za kucheleweshwa, rasimu ya karibuni kabisa iliyoonyeshwa shirika la habari la AFP inatoa wito wa hatua za dharura ili kuruhusu maramoja shughuli za kiutu kwa njia salama, na pia kutengeneza mazingira ya kuwepo mpango endelevu wa usitishwaji wauhasama. Hata hivyo haitoi wito wa usitishwaji maramoja wa mapigano. Balozi wa Marekani Linda Thomas-Greenfield aliwaambia waandishi habari jana usiku kuwa kama azimio hilo litawasilishwa kama lilivyo, basi Marekani italiunga mkono. Amekanusha kuwa rasimu ya azimio hilo imedhoofishwa, akisema kuwa bado iko imara na inaliunga mkono kundi la nchi za Kiarabu.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW