1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Azimio laa baraza la usalama la umoja wa mataifa dhidi ya kulazimishwa watoto kutumika vitani

27 Julai 2005

New-York:

Baraza la usalama la umoja wa mataifa limepitisha azimio linalozungumzia mkakati wa kuwalinda watoto katika nchi zinazokumbwa na vita vya wenyewe kwa wenyewe.Azimio hilo linazungumzia vikwazo dhidi ya pande zinazohasimiana zitakazowatumia watoto vitani au zitakazokwenda kinyume na sheria za kimataifa za kuwalinda watoto nyakati za vita.Mbali na watoto kuuliwa vitani,sheria hizo zinapiga marufuku pia watoto ,kutekwa nyara,kuingiliwa kwa nguvu kimwili na kulazimishwa kupigana vita.Azimio la baraza la usalama linazungumzia marufuku ya kupatiwa silaha,kusafiri na vikwazo vya fedha kwa nchi au kundi lolote litakalokwenda kinyume na sheria hizo.
Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW