1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
MigogoroSyria

Baada ya Syria, je, utawala wa Iran utafuata na kuanguka?

John Juma Amir Soltanzadeh
17 Desemba 2024

Kwa wapinzani Iran, kuporomoka kwa utawala wa Bashar al-Assad ni muhimu kwa sababu Syria imekuwa msingi wa kimkakati kwa Iran katika kanda hiyo. Baada ya anguko la Assad huko Syria, je utawala wa Iran pia utaanguka?

Iran I Kiongozi wa kidini Ayatollah Ali Khamenei
Matukio nchini Syria yaibua wasiwasi kote Iran, hata kumfanya Khamenei kutoa taarifa kwa umma.Picha: Office of the Iranian Supreme Leader/AP/picture alliance

Kuporomoka kwa utawala wa Bashar al-Assad nchini Syria, kumepokelewa kwa mchanganyiko wa matumaini na tahadhari. Wengi wa wapinzani ndani ya Iran waliokatishwa tamaa na utawala wao wa kimabavu wa uongozi wa Kiislamu, wanalinganisha uwiano kati ya mapambano yao na ya watu wa Syria.

Kwa raia wengi wa Iran, Syria imekuwa msingi wa mkakati wa kikanda wa Tehran, ikiashiria sio tu ushawishi wa kijiografia lakini pia mfano wa pamoja wa ustahimilivu dhidi ya utawala wa kimabavu.

Kwa hivyo, matukio ndani ya Syria yanahisiwa katika nyanja zote ikiwemo ya kijamii na kisiasa ndani ya Iran.

Kuondolewa kwa Assad kumefufua matumaini miongoni mwa Wairani wapinzani, kuhusu uwezekano wa kutokea mabadiliko nchini mwao, hasa baada ya serikali ya Iran kulikandamiza kikatili vuguvugu lililotetea haki na uhuru wa wanawake. Ukandamizaji uliosababisha vifo vya mamia na maelfu ya wengine kufungwa jela.

Soma pia: Iran yawanyonga zaidi ya watu 400 mwaka 2024

Hali hiyo hata ilimlazimisha kiongozi wa kidini Ali Khamenei kutoa taarifa kwa umma.

"Yeyote ambaye tathmini yake au kauli zake zinawadhuru watu, anafanya kosa la jinai na atakabiliwa vilivyo. Baadhi wanafanya haya wakiwa ughaibuni kutumia vyombo vya habari vinavyotangaza kwa lugha ya Kifursi. Yeyote humu nchini asithubutu kuhusika na matendo kama hayo,” alisema Khamenei wiki iliyopita.

Meza ya Duara: Anguko la Assad na mustakbali wa Syria

This browser does not support the audio element.

Khamenei aonyesha wasiwasi wa athari za matukio ya Syria

Kauli yake inasisitiza wasiwasi wa serikali yake kuhusu athari kubwa, hasa ikizingatiwa kuondolewa kwa Assad kunaonyesha udhaifu katika tawala zinazokandamiza upinzani na kutegemea sana uungwaji mkono kutoka nje.

Uongozi wa Iran unaweza kuhofia kwamba matukio kama hayo yanayovuruga utulivu, yanayosababisha hali ngumu ya uchumi na yanayodhoofisha ushirikiano wa kikanda, pia yanaweza kujitokeza nchini humo na kutishia amani ya nchi.

Unaweza kusoma pia: EU kutuma mjumbe kuzungumza na viongozi wapya wa Syria

Hossein Razzagh, mwanaharakati wa kisiasa na mfungwa wa zamani, ambaye amekuwa akizuiliwa mara kwa mara tangu maandamano ya Vuguvugu la Kijani la mwaka 2009, anaamini kwamba kuanguka kwa Assad, kimsingi, kumewakosesha amani waungaji mkono shupavu wa utawala wa Iran.

Aghalabu, waungaji mkono hao huwa familia za maafisa serikalini, wenye mafungamano na maafisa wa jeshi, wakuu wa kidini na wanaowekeza pakubwa kuhakikisha utawala unasalia madarakani. Lakini sasa anguko la mshirika wao muhimu nchini Syria limewaacha wakiwa wametishika.

Assad akimbia nchi, waasi waukamata Damascus

01:45

This browser does not support the video element.

"Mashine ya propaganda ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran" imetikiswa

Akizungumza na DW, Razzagh ameangazia kauli za familia ambazo zilipoteza jamaa zao, wakipigana vikali nchini Syria, kulinda utawala wa Bashar al-Assad maarufu kama "Watetezi wa Madhabahu" na kusema anguko la Assad limewaacha wafuasi wenye misimamo mikali kwenye mshtuko mkubwa.

Unaweza kusoma pia: Mjumbe wa UN Syria ataka vikwazo viondolewe baada ya Assad

Razzagh, amesema matukio nchini Syria yamekitikisa kile alichokiita "Mashine ya propaganda ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran" na kwamba wafuasi wake sugu wanajiuliza ikiwa Iran yenyewe ipo ukingo wa kuporomoka.

Ameongeza kuwa hali ya sasa ya utawala wa Iran kupoteza uaminifu miongoni mwa wafuasi wake ni jambo ambalo halijawahi kutokea, hata ikilinganishwa na matukio kama vile Vuguvugu la Kijani la mwaka 2009, maandamano ya mafuta ya 2019, au matukio ya baada ya kuangushwa kwa ndege ya kimataifa ya Ukraine.

Kulingana na Razzagh, hali ya kisaikolojia ya jamii, ni kwamba cheche yoyote, iwe kifo cha Khamenei au shida yoyote kubwa, inaweza kuashiria mwanzo wa mwisho wa utawala wa Iran.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW