1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Baadhi ya makundi DRC yapinga kikosi cha Afrika Mashariki

23 Juni 2022

Viongozi wa baadhi ya makundi ya wapiganaji mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo wametangaza kupinga mpango wa kupelekwa kikosi cha jeshi nchini humo chini ya mwavuli wa Jumuiya ya Afrika Mashariki.

DR Kongo | Soldaten in einer Militäroperation gegen bewaffnete Kräfte
Picha: Alain Uaykani/Xinhua/picture alliance

Viongozi wa baadhi ya makundi ya wapiganaji mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo wametanga kupinga mpango wa kupelekwa kikosi cha jeshi nchini humo chini ya mwavuli wa Jumuiya ya Afrika Mashariki.

Viongozi hao ikiwemo kutoka kundi la wapiganaji la Mai Mai wanapinga mpango huo wakisema utaligawa taifa. 

Majuma machache baada ya kuzuka upya kwa mapigano kati ya jeshi la Kongo na  waasi wa M23, mamia ya vijana wengine kutoka makundi ya kizalendo yameonekana kuimarisha ngome zao ndani ya misitu wilayani Rutshuru huku wakidai kuwa tayari kukabiliana na kundi hili la uasi lililo faulu kuuteka mji mdogo wa Bunagana mapema mwanzoni mwa juma lililopita.

Mwanajeshi wa jeshi la Kongo FARDCPicha: Alexis Huguet/AFP/Getty Images

Baadhi ya makundi yapinga mpango uliotiwa saini Nairobi

Hatua hii ya vijana wazalendo ambayo inaweza kuyatumbukiza maeneo hayo katika mgogoro wa muda mrefu  sasa ,imejiri siku chache tu baada ya viongozi wa nchi za jumuiya ya afrika mashariki kutangaza azma ya kutuma kikosi maalumu hapa mashariki ya Kongo kitakachokabiliana na makundi ya waasi ikiwemo hilo la M23 linaloshukiwa kupata msaada wa nchi jirani ya Rwanda.

Hata hivyo mpango huo tayari unapingwa na baadhi ya makundi ya wapiganaji wa kizalendo ambao wameahidi kupambana na kila atakaye washambulia.

Vyanzo kutoka mashirika ya kiraia, vimethibitisha kua bado mapigano yaliendelea hadi Jumatano jioni katika vijiji vya Ruvumu , Bikenge na  Bweza  katika wilaya ya Rutshuru ambako jeshi la Kongo liliendelea kurusha makombora kuelekea ngome za M23.

Wakimbizi katika eneo la BunaganaPicha: Emmanuel Lubega/DW

Jeshi la Afrika Mashariki litaigawa Kongo

Wakati hayo yakijiri, makundi mengine  ya wapiganaji wanaopiga kambi katika milima ya uvira huko Kivu Kusini wamedai pia kupinga kuwasili kwa kikosi hicho cha kikanda kufuatia kile wanachokiita kuwa njama ya kuligawana taifa la Kongo.

Tangu kuingia madarakani kwake Rais Felix Tshisekedi mwaka wa 2019, jeshi la Kongo halijawacha kupambana na makundi ya waasi ambayo yameendelea kukwamisha maendeleo ya raia.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW