1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Baadhi ya mashambulio dhidi ya Urusi yanatokea ndani

22 Agosti 2023

Shirika la ujasusi la Uingereza limesema baadhi ya mashambulio dhidi ya Urusi yanayofanywa kwa ndege zisizo na rubani yanatokea ndani ya nchi hiyo.

Sehemu ya jengo lililoharibiwa na shambulizi kutumia ndege isiyokuwa na rubani. Agosti 1, 2023.
Sehemu ya jengo lililoharibiwa na shambulizi kutumia ndege isiyokuwa na rubani. Agosti 1, 2023.Picha: EVGENIA NOVOZHENINA/REUTERS

Wizara ya ulinzi ya Uingereza imerelejea hasa shambulio la mwishoni mwa wiki iliyopita kwenye mji wa Novgorod ulio umbali wa kilometa 650 kutoka kwenye mpaka wa Urusi na Ukraine.

Wakati huo huo Urusi imesema imeiteketeza mashua ya upelelezi ya Ukraine kwenye bahari nyeusi.

Mnamo siku za karibuni Urusi imekuwa inailaumu Ukraine kwa kufanya mashambulio ndani ya ardhi yake tangu Ukraine ianze juhudi za kuyakomboa maeneo yake.

Katika kadhia nyingine Urusi imesema leo ilizitungua ndege za droni za Ukraine katika anga ya mji wa Moscow.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW