1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Vijana hawajaridhishwa na Ruto kulivunja baraza la mawaziri

12 Julai 2024

Baadhi ya vijana nchini Kenya bado hawajaridhishwa na hatua ya Rais William Ruto ya kulivunja mbali baraza lake la mawaziri, huku wengine wakitahadharisha kwamba wataanza tena kufanya maandamano asipojiuzulu kama rais.

Rais wa Kenya  William Ruto
Rais wa Kenya William RutoPicha: Simon Maina/AFP

Baadhi ya vijana nchini Kenya bado hawajaridhishwa na hatua ya Rais William Ruto ya kulivunjilia mbali baraza lake la mawaziri, huku wengine wakitahadharisha kwamba wataanza tena kufanya maandamano asipojiuzulu kama rais. Katika hatua ya kutuliza hali, Ruto hapo jana aliwafuta kazi mawaziri wake wote akiwemo Mwanasheria Mkuu, isipokuwa makamu wa rais Rigathi Gachagua na waziri kiongozi ambaye pia ni waziri wa mambo ya nje Musalia Mudavadi. Wachambuzi wanasema hatua hiyo inatoa fursa ya mwanzo mpya ila wameonya kwamba kuhusiana na uwezekano wa athari zaidi. Rais huyo wa kenya amekuwa na wakati mgumu kukabiliana na maandamano yanayopinga nyongeza ya kodi na yaliyosababisha vifo vya watu kadhaa. Maandamano hayo yalipangwa na vijana nchini humo kupitia mitandao ya kijamii.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW