Baadhi ya Wabunge wataka waziri mkuu wa Ugiriki ajiuzulu
2 Novemba 2011Matangazo
Mbunge mmoja wa Kisoshalisti alisaliti chama chake, mwingine kutaka uitishwe uchaguzi wa mapema na wa tatu kutaka kuundwe serikali ya muda itakayojumuisha vyama vyote kwa ajili ya kuulinda mpango wa Umoja wa Ulaya. Wengine kadhaa walitaka waziri mkuu huyo ajiuzulu. Bunge la Papandreou lenye uwakilishi mkubwa hivi sasa limekalia ncha kali ya kisu likiwa na kiasi ya manaibu 152 katika viti 300 vya ubunge. Tarehe kamili ya kura ya maoni bado haijapangwa lakini mawaziri wanasema inatarajiwa kufanyika mapema mwaka ujao.