Baadhi ya wakaazi wazuiwa kujiandikisha kama wapiga kura DRC
3 Februari 2023Wakati tume ya uchaguzi nchini Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo ikiendelea na zoezi la kurekebisha daftari la wapigakura, baadhi ya wakaazi wa mji wa Kalemie wamejikuta wakinyimwa haki ya kujiandikisha kwenye daftari hilo kwa kudaiwa kutokuwa raia halisi wa Kongo.
Lakini pia raia wanawalalamikia watumishi wa tume hiyo ya CENI.
Kila kukicha, raia wanajitokeza kwa wingi kujiandikisha kwenye daftari la wapiga kura. Vituo 25 vimetengwa mjini Kalemie kwaajili ya kujiandikisha, miongoni mwa vituo hivyo ni Kichanga, ambako raia wenye asili ya Rwanda wametolewa kwenye foleni na wakaazi wa Kalemie kwa madai kuwa hawastahili kupata kitambulisho hicho.
Upande wao mashirika ya kiraia mjini Kalemie kupitia kiongozi wao Byaese Issa wamewaomba raia wenye asili ya kigeni kufuata sheria za nchi Ili kupata uraia wa cchi hii.
Upinzani wakosoa zoezi la usajili wa wapigakura nchini Congo
Wakati hayo yakitokea, raia wa mjini Kalemie wanalalamikia namna maafisa wa tume huru ya uchaguzi CENI wanavyofanya kazi, kwa kuwapa vitambulisho watu ambao hawajafuata utaratibu
Ikumbukwe kuwa utowaji wa vitambulisho hivyo utadumu kwa muda wa mwezi mmoja
Zuberi Ally DW, kalemie DRC