1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Baba Mtakatifu akumbuka mauwaji ya halaiki Rwanda:

28 Machi 2004

ROMA:
Baba Mtakatifu John Paul II hii leo aliyakumbuka yale mauwaji ya halaiki yalitokea miaka kumi iliyopita nchini Rwanda. Katika mahubiri yake kwenye Uwanja wa Mtakatifu Peter mjini Roma Baba Mtakatifu aliita Jumuiya ya Kimataifa kuongeza juhudi zake za amani katika Afrika ya Kati. Isijiachiliye kuvunjwa moyo bali inapaswa kuunda ustaarabu wa upendo huko Afrika ya Kati. Kwa mara nyingine naye Katibu Mkuu wa UM Kofi Annan alitamka masikitiko yake kwamba Jamii ya Kimataifa ilishindwa kuingilia kati wakati wa mauwaji ya halaiki ya Rwnada.- Nayo Rwanda inataka kuwaachilia huru wafungwa si chini ya 30,000 hadi mwishoni mwa Juni. Wafungwa hao walikiri kushiriki katika mauwaji hayo ya halaiki.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW