Baba Mtakatifu anyooshea kidole utoaji mimba
10 Mei 2007Kiongozi huyo mkuu wa kanisa katoliki duniani mwenye umri wa miaka 80 alisema kuwa hatoshindwa katika kusisitiza umuhimu wa kuchukua hatua kuhakikisha kuwa msingi imara wa familia unaimarishwa.
Aidha ameshutumu utoaji mimba, akitolea mfano umuhimu wa kuhamasisha kuheshimu na kuthamini maisha toka pale mimba inapotungwa hadi kifo cha kawaida kinapotokea.
Karibu nusu ya waumini billioni 1.1 wa kanisa la katoliki duniani wako America ya Kusini, huku Brazil ikiwa na idadi kubwa.Hata hivyo katika miaka ya hivi karibuni kanisa hilo limekuwa likipoteza waumini wengi.
Asilimi 64 ya Wabrazil ni wakatoliki, lakini idadi hiyo imepungua sana katika moungo mmoja uliyopita, huku dini nyingine za kiinjili kutoka Marekani zikizidi kuimarika kwa asilimia 17.
Kanisa Katoliki pia lilipoteza mapambano muhimu nchini Mexico wakati jiji la Mexico lilipotangaza kuruhusu utoaji mimba.
Akizungumza na waandishi wa habari wakati akieleka Brazil, Baba Mtakatifu aliunga mkono tishio la maaskofu wa Mexico, kuwatenga wabunge wa jiji hilo waliyopitia sheria ya kuruhusu utoaji mimba.
Jiji la Mexico ni moja kati ya miji michache katika America ya Kusini ambapo utoaji mimba umeruhusiwa katika miezi mitatu ya mwanzo ya mimba hiyo
Papa Benedictor wa 16 muda mfupi ujayo anatarajiwa kuwahutubia vijana kiasi cha elfu 40 kutoka pembe zote za America ya Kusini waliyojazana katika uwanja wa mpira mjini Sao Paulo.
Baadaye atakuwa na mazungumzo na Rais wa Brazil nchi ambayo kwa sasa iko katika mjadala wa utoaji mimba.