1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Baba Mtakatifu Benekidt wa 16 ataka mapigano yasimamishwe nchini Libya

Abdu Said Mtullya27 Machi 2011

Baba Mtakatifu atoa mwito wa kukomesha umwagikaji damu nchini Libya

Baba Mtakatifu Benedikt wa 16Picha: AP

Wapinzani wa Kanali Gaddafi wameingia katika mji wa kusafirishia mafuta - Ras Lanus leo baada ya kuwatimua wanajeshi wa Gaddafi mashariki mwa Libya.Hata hivyo habari hizo zimetolewa na mpiganaji mmoja wa wapinzani alienukuliwa na shirika la habari la Reuters.

Akizungumza akiwa katika njia ya kuelekea kwenye mji wa Ras Lanus mpiganaji huyo Walid al Arabi aliwakariri wapiganaji wanaompinga Gaddafi waliokuwa wanatoka mji wa Ras Lanus wakisema kuwa hakuna tena jeshi la Gaddafi katika mji huo.

Na habari zaidi zinasema kuwa wapinzani wanasonga mbele kuelekea magharibi.Baada ya kuuteka mji muhimu wa Adjabiya, waandishi wa habari wamethibitisha kuwa waasi pia wameuteka mji wa Brega.

Lakini habari nyingine zinasema kuwa majeshi ya Gaddafi yameanza kuushambulia tena mji wa Misrata.

Wakati huo huo waziri wa ulinzi wa Marekani Robert Gates amepinga wazo la kuuangusha utawala wa Gaddafi na kueleza kuwa hatua hiyo ni ya utata mkubwa.

Baba Mtakatifu Benedikt wa 16 ametoa mwito wa kusimamisha matumizi ya silaha nchini Libya.Mwito huo unayahusu pia majeshi ya nje. Baba Mtakatifu amesema leo mjini Rome kwamba anauelekeza mwito wake kwa taasisi za kimataifa na kwa wote wale wenye mamlaka ya kijeshi na kisiasa.