1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Baba yake Marine Le Pen afariki dunia

7 Januari 2025

Muasisi wa chama cha siasa kali za mrengo wa kulia cha National Front, nchini Ufaransa, Jean-Marie Le Pen amefariki dunia akiwa na umri wa miaka 96.

Ufaransa: Jean-Marie Le Pen akiwa na binti yake Marine Le Pen enzi za uhai wake.
Jean-Marie Le Pen akiwa na binti yake Marine Le Pen enzi za uhai wake.Picha: Valery Hache/AFP/Getty Images

Duru za karibu na mwanawe mwanasiasa huyo mkongwe,Marie Le Pen, zimetoa ripoti juu ya kifo hicho leo Jumanne.

Mwanasiasa Jean Marie Le Pen, aliisaidia kambi ya siasa kali kuzipa mwelekeo mpya siasa za nchini Ufaransa katika kipindi cha miaka 40 ya harakati zake za kisiasa, akiwavutia wapiga kura  wasioridhishwa na sera ya uhamiaji nchini humo pamoja na  usalama wa ajira.

Soma pia: Ufaransa: Jean Marie Le Pen afukuzwa kutoka chama chake

Aliwahi kupigania urais mara tano nchini Ufaransa kupitia chama chake cha National Rally ambapo mwaka 2002 aliigia kwenye duru ya pili ya uchaguzi na kushindwa na Jacques Chirac aliyechaguliwa kwa kishindo.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW