1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaIndia

Baerbock aendelea na ziara nchini India

6 Desemba 2022

Waziri wa mambo ya nje wa Ujerumani Annalena Baerbock yuko nchini India katika ziara yake ya kwanza ya kiserikali na anataka kushirikiana pamoja na India kuendeleza mapambano dhidi ya mabadiliko ya tabia nchi.

Indien Neu Delhi | Außenministerin Baerbock und Außenminister Subrahmanyam Jaishankar
Picha: Carsten Koall/dpa/picture alliance

Mwanadiplomasia huyo wa ngazi ya juu wa Ujerumani ameuambia mkutano uliofanyika huko New Delhi kuhusu vipaumbele vya Ujerumani katika eneo hilo, kwamba mgogoro wa mazingira ni kitisho kikubwa katika karne hii kwa ulimwengu mzima.

India Alhamisi iliyopita ilichukua uongozi wa kundi la nchi tajiri na zinazoinukia kiuchumi la G20 na waziri wa mambo ya nje wa Ujerumani amesema kauli mbiu ya uongozi huo wa India, ambayo ni dunia moja mustakabali wa pamoja, inaakisi namna ambavyo ulimwengu unaweza kuukabili mustakabali huu kwa pamoja ikiwa tu utakuwepo ushirikiano.

Baadaye leo amepanga kukitembelea kijiji cha Khori kilichoko nje ya mji wa New Delhi kukutana na mkuu wa shirika moja lisilo la kiserikali linalojihusisha na masuala ya kutoa huduma za kibenki kwa watu wasiokuwa na kipato kikubwa, masuala ya nishati endelevu, upandaji miti, kuwawezesha wanawake nchini India.