1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
MigogoroUjerumani

Baerbock afanya mazungumzo na maafisa wa Israel

6 Septemba 2024

Waziri wa Mambo ya Nje wa Ujerumani Annalena Baerbock yuko nchini Israel hii leo baada ya ziara yake nchini Saudi Arabia na Jordan.

Ziara ya Annalena Baerbock nchini Ivory Coast
Waziri wa Mambo ya Nje wa Ujerumani Annalena Baerbock akiwa na Waziri wa Mambo ya Nje wa Ivory Coast Kacou Houadja Leon Adom na Balozi wa Ujerumani nchini Ivory Coast Matthias VeltinPicha: Luc Gnago/REUTERS

Baerbock amekutana na Waziri wa Mambo ya Nje wa Israel, Israel Katz, mjini Tel Aviv mapema leo na hapo baadaye atakutana Waziri wa Ulinzi Yoav Gallant.  

Aidha anatarajiwa kwenda kwenye Ukingo wa Magharibi unaokaliwa kimabavu na Israel kukutana na Waziri Mkuu wa Mamlaka ya Palestina, Mohammed Mustafa, mjini Ramallah.

Soma pia: Baerbock aunga mkono msaada zaidi wa kijeshi kwa Ukraine 

Baerbock amesema anaamini kwamba Mamlaka hiyo inaweza kuwa na mchango muhimu katika serikali ya baada ya vita vinavyoendelea sasa kwenye Ukanda wa Gaza.

Mwanadiplomasia huyo wa ngazi za juu wa Ujerumani yuko Mashariki ya Kati kuhamasisha juhudi za kufikia makubaliano ya kusitisha mapigano, kuachiliwa mateka wa Israel na misaada zaidi kupelekwa Ukanda wa Gaza.