Baerbock afanya ziara ya siku nne Iraq
8 Machi 2023Matangazo
Waziri wa mambo ya nje wa Ujerumani Annalena Baerbock ameahidi usaidizi zaidi wa Ujerumani kwa Irak wakati alipoanza ziara yake ya siku nne nchini humo. Baerbock pia ameahidi kwamba nchi hiyo itaendelea kupokea msaada katika mapambano dhidi ya kundi la kigaidi linalojiita Dola la Kiislamu, IS.Waziri wa mambo ya nje wa Ujerumani ziarani Sweden na Finland
Waziri huyo pia ameikosoa pakubwa Iran akiitaka nchi hiyo kusitisha mashambulizi yake ya makombora kwa Irak. Waziri huyo wa mambo ya nje wa Ujerumani ameyasema haya mjini Baghdad baada ya kukutana na waziri wa mambo ya nje Fuad Hussein. amepangiwa kukutana na viongozi wa Kikurdi huko Erbil leo.