1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Baerbock aitaka UN kusimamia usitishwaji mapigano Yemen

16 Mei 2023

Waziri wa Mambo ya nje wa Ujerumani Annalena Baerbock ambaye yupo ziarani nchini Saudia Arabia amesema kuwa mchakato wa usitishwaji mapigano nchini Yemen ni lazima usimamiwe na Umoja wa Mataifa.

Schweden | informelles Treffen der EU-Außenminister in Stockholm
Picha: Kira Hofmann/photothek/picture alliance

Baada ya mkutano na mwenzake wa Yemen Ahmed bin Mubarak katika mji wa Jeddah huko Saudia, Bi Baerbock amesema hatua hiyo itakuwa muhimu kwa amani ya kudumu na hali ya utulivu katika taifa hilo linalokumbwa na vita.

AKiwa nchini humo, Baerbock alikutana pia na Mratibu wa Umoja wa Mataifa kwa Yemen, David Gressly, na kujadili kuhusu janga la kibinadamu katika taifa hilo la Kiarabu na nchi maskini zaidi baada ya miaka minane ya vita vya wenyewe kwa wenyewe.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW