Baerbock amuita balozi wa Urusi
18 Aprili 2024Matangazo
Kulingana na polisi ya Ujerumani, watu hao wawili walikamatwa siku ya Jumatano (Aprili 17) katika jimbo la Bavaria kusini mwa Ujerumani wakidaiwa kuwa katika harakati za ujasusi kwa ajili ya Urusi na kutafuta sehemu za kufanya mashambulizi ndani ya ardhi ya Ujerumani.
Soma zaidi: Naibu Kansela wa Ujerumani afanya ziara ya ghafla Ukraine
Baada ya kukamatwa kwa watu hao, Waziri wa Mambo ya Ndani wa Ujerumani, Nancy Faeser, alisema Ujerumani isingelitishwa na majaribio ya kijasusi ya Urusi.