1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Baerbock: Mazungumzo magumu kuhusu mazingira yanahitajika

17 Novemba 2025

Rais wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa Annalena Baerbock, amesema kuna haja ya mabadiliko katika majadiliano magumu katika mkutano wa Mazingira wa Umoja wa Mataifa wa COP30.

Rais wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa Annalena Baerbock
Rais wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa Annalena Baerbock, amesema kuna haja ya kuwa na mazungumzo magumu kuhusu mazingira Picha: Ibraheem Abu Mustafa/REUTERS

Baerbock, ambae pia ni waziri wa zamani wa mambo ya nje wa Ujerumani amesema ni muhimu kwa masilahi binafsi ya taasisi kufanya mabdiliko.

Wajumbe katika mkutano wa COP30, kutoka mataifa takriban 200 bado wanajadili hadi mwisho wa wiki hii namna ya kupunguza ongezeko la joto duniani hadi kufikia nyuzi joto 1.5 katika kipimo cha Celcius ukilinganisha na viwango vya kabla ya mapinduzi ya kiviwanda.

Wanasayansi wanasema kufikiwa kiwango hicho ni muhimu ili dunia ijikinge na madhara makubwa yatokanayo na mabadiliko ya tabia nchi. 

 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW