1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaUrusi

Baerbock awasili Japan kwa mkutano wa G7

16 Aprili 2023

Waziri wa mambo ya nje wa Ujerumani Annalena Baerbock amewasili nchini Japan kwa ajili ya kikao cha mashauriano cha mawaziri wa mambo ya nje ya mataifa yenye nguvu kubwa kiuchumi ulimwenguni ya G7.

Südkorea Annalena Baerbock in der Demilitarisierten Zone
Picha: Kira Hofmann/photothek/IMAGO

Kwenye kikao hichi kitakachoanza baadae jioni hadi siku ya Jumanne, mawaziri hao wa mambo ya nje wa G7 watajadiliana juu ya hatua zaidi katika vita vya Urusi nchini Ukraine na msimamo wao wa pamoja kuelekea hatua za China za kujiimarisha zaidi kimataifa. Mipango ya nyuklia ya Iran huenda pia ikajadiliwa.

Waziri Annalena Baerbock wa Ujerumani amesema mapema leo akiwa Seoul, Korea Kusini kwamba G7 itaendelea kupinga vikali uvamizi wa Urusi nchini Ukraine na kumuonyesha rais Vladimir Putin kwamba hatafanikisha malengo yake kwa namna yoyote ile.

Kikao hicho kinachofanyika katika mji wa Karuizawa ni maandalizi ya mkutano wa kilele wa wakuu wa mataifa hayo utakaofanyika Hiroshima, nchini Japan.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW