1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Baerbock kuelekea Israel baada ya mashambulio la Iran

16 Aprili 2024

Waziri wa Mambo ya Nje wa Ujerumani Annalena Baerbock, anatarajiwa kuelekea Israel jioni ya leo, baada ya shambulizi kubwa la Iran dhidi ya taifa hilo.

Waziri wa Mambo ya Nje wa Ujerumani Annalena Baerbock
Waziri wa Mambo ya Nje wa Ujerumani Annalena BaerbockPicha: Jörg Carstensen/dpa/picture alliance

Kulingana na msemaji wa wizara ya nchi za kigeni wa Ujerumani, Baerbock anatarajiwa kuzungumza na Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu, waziri wa Mambo ya Nje, Israel Katz na waziri asiye na wizara maalum, Benny Gantz kesho Jumatano.

Hofu ya kutokea kwa mgogoro mkubwa katika Mashariki ya Kati imekuwa ikiongezeka kufuatia mashambulizi makubwa ya Iran siku ya Jumamosi.

Soma pia:Iran yaipa onya kali Israel isijaribu kujibu mashambulizi

Iran ilirusha mamia ya makombora na droni kuelekea Israel, lakini nyingi zilizuiwa na Israel pamoja na washirika wake.

Mkuu wa majeshi ya Israel Luteni Jenerali Herzi Halevi amesema shambulizi la Iran litajibiwa.

Viongozi mbalimbali wa ulimwengu wamekuwa wakiihimiza Israel kujizuia kama tahadhari ya kuepusha mzozo kutanuka kote Mashariki ya Kati.