1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
MigogoroUjerumani

Baerbock kufanya ziara Mashariki ya Kati siku ya Jumapili

5 Januari 2024

Waziri wa mambo ya nje wa Ujerumani Annalena Baerbock atafanya ziara kuelekea Israel siku ya Jumapili.

Waziri wa mambo ya nchi za nje wa Ujerumani Annalena Baerbock
Waziri wa mambo ya nchi za nje wa Ujerumani Annalena BaerbockPicha: Sebastian Rau/photothek/picture alliance

Hiyo itakuwa ni ziara yake ya nne nchini humo tangu kuzuka kwa vita kati ya Israel na Hamas katika ukanda wa Gaza.

Baerbock anatarajiwa kufanya mazungumzo na waziri mpya wa mambo ya nje wa Israel, Yisrael Katz pamoja na Rais Isaac Herzog.

Pia atakutana na kiongozi wa mamlaka ya Palestina Mahmud Abbas na waziri wa mambo ya nje wa Palestina Riyad al-Maliki.

Mazungumzo hayo yatajikita juu ya hali ya kibinadamu katika ukanda wa Gaza, hali ya ukingo wa Magharibi, hali tete katika mpaka wa Israel na Lebanon pamoja na juhudi za kuachiliwa huru mateka zaidi.

Baadaye, waziri huyo wa mambo ya nje wa Ujerumani ataelekea nchini Misri kukutana na mwenzake Sameh Shoukry na amepanga pia kuitembelea Lebanon.