Baerbock: Sina nia ya kugombea ukansela
11 Julai 2024Matangazo
Katika matamshi yake yaliyorushwa jana Jumatano kwenye televisheni, Baerbock amesema wajibu wake wa kisiasa kwa sasa ni kuzingatia zaidi masuala ya kidiplomasia wakati huu ambapo kuna migogoro mingi, na sio kampeni za uchaguzi.
Mwanadiplomasia huyo wa Ujerumani amekiambia kituo cha televisheni cha Marekani, CNN kwamba ataendelea kutumia nguvu zake zote kama waziri wa mambo ya nje kujenga uaminifu na ushirikiano kwa sababu washirika wengi duniani kote na Ulaya wanategemea hilo.
Soma pia:Baerbock: weka himizo kwa Israel kujizuia dhidi ya Hezbollah
Baerbock alikuwa mgombea wa kwanza wa ukansela wa chama cha Kijani kinachotetea mazingira, katika uchaguzi wa mwaka 2021, ambapo kilipata matokeo ya kihistoria ya asilimia 14.7 ya kura.