1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Baerbock: Tunatumai Israel itazuia madhila kwa Wapalestina

11 Desemba 2023

Waziri wa mambo ya nje Annalena Baerbock amesema Ujerumani inatarajia Israel kuzingatia mikakati ya kijeshi itakayozuia mateso miongoni mwa raia wa Palestina.

Waziri wa Mambo ya Nje wa Ujerumani, Annalena Baerbock
Waziri wa Mambo ya Nje wa Ujerumani, Annalena BaerbockPicha: Sebastian Rau/photothek/picture alliance

Tamko la waziri huyo linaonesha kubadilika kwa kiasi kwa msimamo wa serikali ya Ujerumani ambayo ilikuwa imejielekeza zaidi katika kuiunga mkono Israel ambayo ni mshirika wake.

Katika mkutano na waandishi wa habari leo mjini Dubai pembezoni mwa mkutano wa Umoja wa Mataifa wa mazingira, Baerbock  amesema Ujerumani inatarajia kuiona Israel ikiruhusu misaada zaidi ya kibinadamu ikiingia na hasa Gaza,na kuhakikisha hatua zake za kijeshi zinaelekezwa zaidi kwa walenga na kuepuka kusababisha mauaji ya raia.

Ujerumani imekuwa ikitetea vikali haki ya Israel kujilinda dhidi ya mashambulizi ya Hamas ya Octoba 7,japo imekuwa ikikabiliwa na ukosoaji ikiwemo na wayahudi wanaoishi Ujerumani, kutokana na mgogoro wa kibinadamu uliosababishwa Gaza.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW