1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Baerbock: Ujerumani kushirikiana na Australia kiusalama

4 Mei 2024

Waziri wa Mambo ya Nje wa Ujerumani Annalena Baerbock ameonesha nia ya kupanua zaidi ushirikiano wa kiulinzi na Australia. Hayo ameyaweka wazi katika siku ya kwanza ya safari yake nchini humo.

Australia Adelaide 2024 | Mawaziri wa Mambo ya Nje Baerbock & Wong katika mkutano na waandishi wa habari
Waziri wa Mambo ya Nje wa Australia Penny Wong (kulia) akiwa na Waziri wa Mambo ya Nje wa Ujerumani Annalena Baerbock wakiwasili kwa mkutano na waandishi wa habari, Mei 3, 2024.Picha: Michael Errey/POOL/AFP/Getty Images

Hata hivyo, hakutaja miradi yoyote maalum  baada ya kukutana na mwenzake Penny Wong huko Adelaide, Australia Kusini, ingawa alionekana kusisitiza ushirikiano wa kiusalama baina ya mataifa hayo mawili.

Ameongeza kusema kwa ujumla mataifa yote mawili yapo katika hali fikra moja ya vitisho vyenye kufanana akitolea mfano, vitisho kutoka Urusi kwa Ulaya na China kwa Australia. Australia ndio kituo cha kwanza kwa safari ya wiki moja ya Baerbock katika eneo la Indo-Pasifiki.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW