1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

BAGDAD: Ajali ya ndege

31 Mei 2005

Marekani imesema kwamba ndege ya kijeshi ya Irak imeanguka kutokana na sababu zisizofahamika. Wanajeshi wanne wa Marekani na mwiraki mmoja wanasadikiwa kuwa wamekufa katika ajali hiyo iliyotokea mashariki mwa Irak.

Wakati huo huo washambuliaji wawili wa kujitoa mhanga wameua watu 27 na kuwajeruhi wengine zaidi ya mia moja katika mji wa Hilla kusini mwa Bagdad.

Shambulio hilo limefanyika wakati ambapo maalfu ya askari wa Irak wakishirikiana na majeshi ya Marekani wanaendesha kampeni kubwa kwa lengo la kuuvunja upinzani.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW