1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

BAGHDAD: Mripuko wa bomu umeua watu 30 nchini Iraq

29 Juni 2007

Watu 30 wameuawa na 50 wengine wamejeruhiwa baada ya bomu lililotegwa ndani ya gari,kuripuka katika mji mkuu wa Iraq,Baghdad.Kwa mujibu wa polisi, mripuko huo ulitokea karibu na kituo cha basi kinachotumiwa sana,kusini-magharibi ya Baghdad. Hapo awali,polisi waligundua miili 20 iliyokatwa vichwa na kutupwa kwenye ukingo wa mto Tigris kusini mwa mji mkuu.Maiti zote ni za wanaume na bado hazijatambuliwa.Inakisiwa walikuwa kati ya miaka 20 na 40.Wakati huo huo,wanajeshi 3 wa Uingereza wameuawa na mmoja amejeruhiwa katika shambulio jingine la bomu katika mji wa Basra,kusini mwa Iraq.