BAGHDAD: Usalama waimarishwa nchini Irak
13 Oktoba 2005Matangazo
Wanajeshi wa Marekani na Irak wameongeza juhudi zao kulinda usalama katika maeneo yote ya Irak, katika juhudi za kupunguza mashambulio ya wapiganaji yanayolenga kuivuruga kura ya maoni juu ya mswada wa katiba mpya, iliyopangwa kufanyika Jumamosi ijayo.
Siku moja baada ya bunge kukubaliana kuufanyia marekebisho mswada huo baada ya uchaguzi utakaofanyika mwezi Disemba, mji wa Baghdad umekuwa na utulivu huku siku kuu ya kitafa ya siku nne ikinza nchini humo. Msako umetangazwa, mipaka ya Irak itafungwa hapo kesho na hakuna atakayeruhusiwa kusafiri kutoka mkoa mmoja hadi mwingine.
Wanajeshi wameendelea kuwakasa wanamgambo mjini Baghdad na vitongonji vyake na wanajenga kuta kuzunguka vituo vya kupigia kura kama vile shule.