BAGHDAD: Vikosi vya Marekani vimeua polisi 6 wa Kiiraki
13 Julai 2007Matangazo
Si chini ya maafisa 6 wa polisi wa Kiiraki na watu 7 wengine wanaoshukiwa kuwa wanamgambo, wameuawa na vikosi vya Marekani katika uvamizi uliofanywa wakati wa alfajiri,mashariki mwa mji mkuu Baghdad.Wanajeshi wa Marekani wamesema, wakati wa operesheni hiyo,wamemkamata afisa wa polisi anaetuhumiwa kuhusika na wanamgambo. Wakaongezea kuwa mapambano yalizuka baada ya vikosi vya Marekani kulengwa na kushambuliwa kutoka kituo cha ukaguzi cha polisi,mapaa ya nyumba na kanisa lililo karibu na hapo.