BAGHDAD: Wakurdi wahimizwa kuwa mfano wa udemokrasia nchini Iraq
4 Juni 2005Matangazo
Rais Jalal Talabani wa Iraq ambae ni Mkurdi,amekihotubia kikao cha kwanza cha bunge huru la Wakurd.Talabani amewataka wabunge hao wawe na mfumo wa kisiasa unaofuata demokrasia katika nchi inayokabiliwa na kitisho cha mgogoro wa kikabila.Amesema,Iraq hivi sasa inapitia wakati ulio muhimu sana katika historia yake.