1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

BAGHDAD: Wanajeshi washtakiwa ubakaji na mauaji

9 Julai 2006

Wanajeshi 4 wa Kimarekani wameshtakiwa ubakaji na mauaji ya kijana wa kike wa Kiiraqi na kuiuwa pia familia yake.Wanajeshi hao walio kazini nchini Irak,wameshtakiwa kupanga njama na mwanajeshi wa zamani Steven Green kufanya uhalifu huo mjini Mahmoudiya,kusini mwa Baghdad.Green,aliezuiliwa Marekani ameyakataa mashtaka ya ubakaji na mauaji.Jeshi la Marekani limearifu kuwa sasa ni Wamarekani 5 walioshtakiwa kuhusika na vifo vinne vilivyotokea mwezi wa Machi.Mwanajeshi wa tano alifunguliwa mashtaka siku ya Jumamosi kuwa alikosa kutimiza wajibu wake kwa vile hakuiripoti kesi hiyo.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW