1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

BAGHDAD: Watekaji nyara watishia kumuua mateka wa Ujerumani

11 Septemba 2007

Kundi la wapiganaji nchini Irak limetishia kumuua mateka wa Ujerumani ikiwa serikali ya mjini Berlin haitawaondoa wanajeshi wake walio Afghansitan katika kipindi cha siku kumi zijazo.

Ukanda wa video uliotumwa katika mtandao wa internet umemuonyesha Sinan Krause akinywa chai akiwa amekaa.

Kundi la kiislamu lisilojulikana linalojiita Arrows of Righteosness, yaani mishale ya haki, lilimteka nyara mwanamume huyo muiraki mwenye asili ya Ujerumani pamoja na mamake mjerumani mnamo mwezi Machi mwaka huu.

Watekaji nyara wa kundi hilo lakini walimuchia huru mwanamke huyo mnamo mwezi Julai kwa sababu alikubali kusilimu.