1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Baghdad. Watu 100 huuwawa kila siku nchini Iraq.

5 Oktoba 2006

Maafisa wa kijeshi wa Marekani wamesema kuwa mashambulizi ya mabomu mjini Baghdad yameongezeka kwa kiwango cha juu.

Matamshi hayo yametolewa wakati kikosi kizima cha jeshi la polisi kimeondolewa katika mitaa kutokana na wasi wasi wa kuhusika na vikundi vya mauaji vya kimadhehebu.

Zaidi ya hayo , maelfu ya polisi wanakabiliwa na uhakiki wa kihalifu, kusema uongo, kama sehemu ya hatua za kuwaondoa wapiganaji ndani ya jeshi hilo.

Hatua hiyo inakuja baada ya watu 40 kutekwa nyara na kundi la watu wenye silaha mjini Baghdad mapema wiki hii.

Siku ya Jumanne waziri mkuu Nuri al-Maliki amezindua mpango uliokubalika na viongozi wa Wasunni na Washia kujaribu kudhibiti hali ya ghasia. Watu wanaokadiriwa kufikia 100 wanauwawa nchini Iraq kila siku.