BAGHDAD: Waziri wa ulinzi wa Marekani afanya ziara ya ghafula Iraq
16 Juni 2007Matangazo
Waziri wa ulinzi wa Marekani,Robert Gates amewasili mji mkuu wa Iraq,Baghdad kwa ziara ya ghafula na amekutana na makamanda wa majeshi ya Marekani.Alipozungumza na waandishi wa habari, Gates alisema,hakuridhika na utendaji kazi wa serikali ya Waziri Mkuu Nouri al-Maliki.Waziri Gates anatazamiwa kumuhimiza al-Maliki kujitahidi zaidi kuleta upatanisho kati ya jamii hasimu na kukomesha machafuko ya kimadhehebu na kushauri kuwa jamii zote zinufaike na mauzo ya mafuta.