1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

BAGHDAD:59 wauawa nchini Iraq

27 Septemba 2007

Watu 59 wameuawa na wengine zaidi ya 130 wamejeruhiwa kutokana na mashambulizi ya mabomu nchini Iraq yaliyofanywa na wanamgambo wanaohisiwa kuwa wa kundi la al Qaida.

Watu 32 waliuawa wakati mabomu mawili ya kutegwa kwenye gari yalipolipuka huko kusini magharibi mwa Baghdad kwenye mji unaokaliwa na washia wengi.

Wakati huo huo jeshi la Iraq limewakamata watu 20 wa chuo cha kijeshi mjini Baghdad wakiwemo maafisa wa ngazi ya juu wakihisiwa kuhusika na utekaji pamoja na mauaji.

Waziri Mkuu wa Iraq Nuri al- Maliki akihutubia katika mkutano wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa mjini New York amesema kuwa nchi hiyo ina safari ndefu ya kufikia hali ya utulivu.

Waziri Mkuu huyo wa Iraq ameonya hali kuwa mbaya zaidi kutokana na kuongeza kwa vitendo vya ghasia na mauaji.

Mjini Washington, Waziri wa Ulinzi wa Marekani Roberts Gates ametaka wizara hiyo ipewe fungu la dola billioni 190 kwa ajili ya vita nchini Iraq na Afghanistan.

Wizara ya Ulinzi imesema kuwa kiwango hicho ni kikubwa kabisa kuwahi kuombwa katika kipindi cha miaka sita ya vita dhidi ya ugaidi.