BAGHDAD:Askari wanane wa Marekani wauawa Irak
8 Oktoba 2005Matangazo
Marekani imesema askari wake wanane wameuawa katika shambulio la mabomu ya kutegwa njiani karibu na miji ya Fallujah na Qaim nchini Irak.
Wakati huo huo majeshi ya Marekani yamemaliza zoezi la siku sita la kuwashughulikia wapinzani nchini Irak ambapo wapinzani zaidi ya 50 waliuawa.
Na majeshi ya Uingereza yamewatia ndani watu 12 ikiwa pamoja na maafisa kadhaa wa polisi kutokana na tuhuma za kuhusika na mashambulio ya mabomu dhidi ya majeshi ya nchi za nje.
Na katika tukio jingine maiti za watu 22 zimekutwa zimefungwa pingu za waya na miili yao imetobolewa na risasi katika mji wa Badra kusini mashariki mwa mji wa Baghdad.