1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

BAGHDAD:Bush asifu hukumu ya kifo dhidi ya Saddam

6 Novemba 2006

Rais Gorge W Bush wa Marekani amepongeza hukumu ya kifo dhidi ya kiongozi wa zamani wa Iraq Saddam hussein akisema kuwa ni mwanzo wa kuelekea demokrasia nchini humo.

Rais Bush amesema ni mafanikio makubwa ya kuondoa utawala wa kidhalimu na kuweka utawala wa kisheria nchini Iraq.

Kiongozi huyo wa zamani wa Iraq Saddam Hussein alikutikana na hatia ya uhalifu dhidi ya binadamu na mahakama inayoungwa mkono na Marekani mjini Baghdad na hivyo kuhukumiwa kunyongwa.

Hata hivyo lakini rais Bush hakuzungumzia moja kwa moja suala hilo la hukumu ya kifo dhidi ya Saddam ambayo imepingwa na Umoja wa Ulaya.

Umoja wa Ulaya umetoa taarifa yake inayosema kwamba inapinga adhabu kubwa kama hiyo katika kesi zote kivyovyote vile na haipasi kutekelezwa dhidi maofisa wa zamani wa Iraq.

Saddam Hussein alishtakiwa dhidi ya mauaji ya washia 148 wa kijiji cha Dujail mwaka 1982 nchini Iraq.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW