BAGHDAD:Damu yaendelea kumwagika Iraq
6 Mei 2007Matangazo
Shambulio la bomu la kutegwa ndani ya gari limeuwa watu takriban 30 na kuwajeruhi wengine 80 karibu na soko lililokuwa na msongamano watu katika mkoa wa Bayya mjini Baghdad.
Shambulio hilo ni moja kati ya mashambulio mabaya kabisa yaliyowahi kutokea mjini Baghdad siku za karibuni.
Wakati huo huo kwenye eneo la Sammara kaskazini mwa Baghdad washambuliaji wawili wa kujitoa muhanga waliendesha gari lilokuwa na mabomu na kushambulia vituo vya polisi ambapo kiasi wairaqi sita waliuwawa na kuwajeruhi wengine wengi.