BAGHDAD:Majeshi ya Marekani yashambulia upya
5 Novemba 2005Matangazo
Majeshi ya Marekani yameanzisha mashambulio mengine katika jimbo la machafuko El Anbar.Kwa mujibu wa msemaji wa majeshi ya Kimarekani,kiasi ya wanajeshi 2,500 wa Kimarekani na 1,000 wa Kiiraqi wanashiriki katika operesheni hiyo.Amesema lengo la mashambulio hayo ni kurejesha hali ya usalama ukingoni mwa mpaka wa Iraq na Syria na pia kuvunja muundo wa mtandao wa kigaidi wa al Qaeda.
