BAGHDAD.Marekani yajenga ukuta kuwatenganisha wairak
22 Aprili 2007Matangazo
Marekani imeanza kujenga ukuta utakaozitenganisha jamii za wasuni na washia katika mji mkuu wa Irak, Baghdad.
Msemaji wa jeshi la Marekani ameeleza kuwa ukuta huo wa kilometa 5 unajengwa ili kuimarisha usalama katika sehemu ambayo imekuwa inashambuliwa mara kwa mara.
Viongozi wa sehemu ambapo ukutwa utajengwa wamelalamika, lakini jenerali mmoja wa Irak amesema lengo la kujenga ukuta huo ni kuwazuia magaidi kufanya mashambulio.